NADHARIA YA TAFSIRI
Nadharia ya tafsiri ninini?

 ni maelezo muhimu kuhusu vipengele mbalimbali vya kifasiri ambavyo vinapaswa kufuatwa au kuzingatiwa na kila mfasiri pindi anapokabiliwa na kazi ya kufasiri.
Kwa ujumla 
Nadharia ya tafsiri ndio nguzo au mhimili muhimu wa shughuli zote za tafsiri. Vipengele vingine vitakavyojadiliwa katika nadharia ya tafsiri ni pamoja na taaluma zinazohusiana na tafsiri na dhima ya nadharia ya tafsiri.
Zipo Sababu za kuanzishwa kwa nadharia za tafsiri.

Newmark (1982), Mwansoko na wenzake (2006) wanasema kuna mambo matatu yaliyosababisha kuanzishwa kwa nadharia ya tafsiri ambayo ni:-
i)          Wingi wa makosa katika tafsiri zilizochapishwa awali; ilionekana kwamba, kulikuwa na makosa mbalimbali kama vile makosa ya kimuundo, kimaumbo, kimsamiati nk. Pia ilikuwa ni nadra/muhali kupata tafsiri zisizokuwa na makosa.
ii)           Kuwepo kwa idadi kubwa (na inayoongezeka) ya asasi zinazojishughulisha na kazi za tafsiri. Hali hii ilisababisha kubuniwa kwa nadharia ya tafsiri ili kuwepo kwa misingi inayokubalika. Mfano; nchini Tanzania peke yake kuna asasi nyingi zinazojishughulisha na tafsiri kama vile: BAKITA,TATAKI, SHIHATA,WAFASIRI na vyombo mbalimbali vya habari kwa mfano:TVMagazeti nk.
iii)       Mfumuko wa istilahi katika taaluma mbalimbali hasa Sayansi na Teknolojia. Hivyo nadharia ya tafsiri ilianzishwa kwa lengo la kuleta ulinganifu wa istilahi hizo kati ya lugha moja na nyingine ili kuwe na ufanisi zaidi.
TAALUMA NYINGINE ZINAZOHUSIANA NA TAFSIRI
Tafsiri inauhusiano mkubwa na taaluma nyingine au vipengele vingine kama ifuatavyo:
Inauhusiano naisimulinganishi; Isimulinganishi hijishughulisha na kulinganisha vipengele mbalimbali vya kiisimu vya lugha mbili au zaidi, pamoja na kuchunguza mbinu za ulinganishi huu. Uhusianao wake na tafsiri;- humsaidia mfasiri kuelewa mifumo ya lugha mbalimbali na jinsi luhga hizo zinavyotumia vipengele vyake vya kiisimu kutolea taarifa mbalimbali.
Inahusiana na isimujamii;- Isimujamii inahusika na kuchunguza uhusiano kati ya lugha fulani na jamii ambayo inatumia lugha hiyo. Rejesta mbalimbali za kijamii pamoja na maingiliano baina ya lugha. Ujuzi wa isimujamii unamsaidia mfasiri kufahamu athari zinazotokana na mahusiano baina ya lugha na jamii husika na kuzingatia mambo mbalimbali katika kutafsiri.
Inauhusiano nasemantiki/pragmatiki;- Semantiki ni taaluma inayochunguza maana ya maneno katika upweke na katika makundi/taaluma inayochunguza maana ya maana. Kwa kuwa kinachotafsiriwa ni mawazo au maana ya matini (siyo neno pwekepweke) basi ujuzi huu wa semantiki utamwezesha mfasiri kujua au kung’amua kuwa maana ya matini hiyo haitokani na maana ya neno mojamoja badala yake inatokana na maana ya kimatumizi kwa ujumla katika mktadha mahususi.
Inauhusiano naelimumitindo (stylistics);- Hii inahusu uainishaji wa mitindo mbalimbali ya lugha na miktadha ya matumizi yake.
Elimumitindo
Mitindo                         Mazingira ya kutumia
Uhusiano wake na tafsiri;- Taaluma hii ya elimumitindo itamwezesha mfasiri kubaini mtindo wa matini chanzi ambao haunabudi kuhamishiwa katika matini lengwa.
Inauhusiano na mantiki (logic);- Mantiki inahusu ukweli na uhakika au usahihi wa mambo kama inavyosemwa, kuandikwa au kuaminika kwa watu. Mantiki humsaidia mfasiri kubaini kauli zisizo dhahiri na zinazokanganya katika matini chanzi ili azirekebishe kwanza kabla ya kuanza kutafsiri. Kwa mfano; The current president of United Republic of Tanzania is Mzee Ally Hassan Mwinyi. Je ni kweli?
NADHARIA YA TAFSIRI
Nadharia ya tafsiri hushughulikia mambo makubwa manne ambayo ndiyo dhima ya nadharia ya tafsiri.

1.  Kubaini na kufasili (define) tatizo la kifasiri yaani kazi au mlolongo wa shughuli za tafsiri zinazopaswa kufanywa katika utatuzi wa tatizo la tafsiri lililobainishwa.
2.  Kuonesha vipengele vyote vinavyopaswa kuzingatiwa katika utatuzi wa tatizo la tafsiri lililobainishwa.
3.  Kuorodhesha taratibu au njia zote zinazowezekana kufanikisha tafsiri inayohusika.
4.    Kupendekeza taratibu zinazofaa zaidi katika kutekeleza zoezi la kufasiri pamoja na mbinu za kutafsiri zilizomuafaka zaidi kwa matini inayohusika.
NADHARIA MAHUSUSI ZA TAFSIRI.
1.  Nadharia ya Usawe wa Kimuundo; nadharia hii inatetewa na mtaalam Catford (1969), Tunapofanya kazi ya kutafsiri tunatakiwa kuzingatia ulinganifu wa kimuundo kati ya matini chanzi na matini lengwa, maana yake ni kwamba muundo wa matini chanzi ujitokeze katika matini lengwa. katika nadharia hii muundo ni muhimu. Pia nadharia hii hutumika zaidi katika kutafsiri maandiko ya kidini hasa Biblia.
2.   Nadharia ya Usawe wa Kidhima; wa tetezi wa nadharia hii ni pamoja na Nida (1964) na Nida na Taber (1969) wanaona kuwa usawe wa kidhima ni muhimu zaidi kuliko usawe wa kimuundo. Wafasiri wanapaswa kuhakikisha kwamba dhima ya matini chanzi pamoja na athari zake zinajitokeza katika matini lengwa. Yaani kama matini chanzi inawalenga watoto inapaswa iandikwe kiasi kwamba watoto wataweza kuelewa. Pia kwa kuzingatia nadharia hii unapaswa kutumia lugha rahisi na inayoeleweka na watu wote. Vilevile tafsiri yako iwe nzuri kiasi kwamba mtu atakaposoma asiweze kujua kwamba hii kazi imetafsiriwa.
3.     Nadharia ya Usawe wa Aina-matini;matini yoyote ile ifasiriwe kwa kuzingatia aina yake. Hii inamaana kwamba kazi itakayotokea itafanana na matini chanzi. Kma matini chanzi ni ya kisheria itakapotafsiriwa matini lengwa nayo itaonekana kuwa ya kisheria. Katika nadharia hii kinachozingatiwa nifani (muundo)namaudhui (dhima/lengo) ya matini yenyewe inayotafsiriwa. Watetezi wa nadharia hii ni Reiss (1971), Buhler (1965) na Newmark (1982/88)
4. Nadharia Changamani (Cross Fertilization theory). Hii ni nadharia tete iliyoasisiwa na P.S.Malangwa (2010) Ndharia hii inadai kwamba huwezi kufanya tafsiri kwa kutumia nadharia moja tu, kwa sababu hakuna nadharia inayojitosheleza yenyewe.
Marejeleo
www.masshele.blogspot.com
Mwansoko (2006)
Namapitio mengine