Kuna ile dhana iliyojengeka kwa baadhi ya watu kwamba mtoto anapozaliwa na utando mweupe kwenye ngozi yake kuwa ni uchafu,na utapewa sababu mbali mbali kwa ni ni kazaliwa mchafu.kuna watakaosema mama yake anakula vitu fulani ambavyo hatakiwi kula na wengine watasema inatokana na mama kufanya mapenzi hadi week za  mwishoni karibia na kujifungua. Hizi zote ni Imani potofu, leo katika makala hii utajifunza kitu hiki ni nini hasa na umuhimu wake.

UTANDO ANAOZALIWA NAO MTOTO NI NINI?
Kitaalamu utando huu unajulikana kama vernix caseosa, ni utando unaosaidia kuikinga ngozi ya mtoto isiharibike. Utando huu unatengenezwa mtoto anapokuwa tumboni na huanza kupungua kuanzia week ya 36 japo baadhi ya watoto utando huu haupungui hadi muda anazaliwa.

UTANDO HUU UNA KAZI GANI?
Kuelewa kazi ya utando huu, fikiria kwanza ngozi yako hasa ya vidole inavojikunja unavokua umeiweka kwenye maji kwa muda,mfano wakati unaoga au unafua lazima itakuwa na makunyanzi.
Maji yanasababisha kitu kama hicho pia hata kwenye ngozi za watoto. Na tukumbuke mtoto anakaa kwenye maji maji ya kwenye mji wa mimba kwa muda wa week 40 basi kipindi chote hiki utando huu unafanya kazi ya kuilinda ngozi ya mtoto isitengeneze makunyanzi na kuwa laini.

FAIDA NYINGINE ZA UTANDO HUU
Mbali na kuwa losheni inayolainisha ngozi ya mtoto utando huu unafanya kazi nyingine zifuatazo:

1.Kumkinga mtoto na maambukizi. utando huu unasaidia kumkinga mtoto na maambukizi ya bakteria,una viambata vinavyozuia radikari huru (ant oxidants) na ant bacteria

2.Inasaidia kuzuia michubuko ya ngozi wakati mtoto anazaliwa. (lubrication)
3.Inasaidia kubalance joto la mtoto.

Mwisho: Tuifute dhana potofu kwamba huu ni uchafu, ni kitu muhimu ambacho kila mtoto anakuwa nacho ili kuikinga ngozi yake dhini ya mambo mbali mbali pindi anapokuwa tumboni na baada ya kuzaliwa