AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

“Tena ngoja nikawaonyeshe kaburi lamke wangu muda kidogo umekwenda”
Tukasimama na tukatoka nje na kuzunguka upande wa pili wa nyumba na gafla nikaanza kumuona Rahma akianza kubadilika sura yake baada ya kuiona picha iliyo wekwa juu ya kaburi la mke wa Mzee Ngoda

ENDELEA
“Huyu ndio mke wangu ambaye alinifanyia mambo mengi ya ajabu sana”
Rahma akapiga magoti taratibu na kuitazama picha kwa kwa umakini huku akiifuta futa vumbi na mimi nikajikutana nikiikazia jicho kwani picha iliyo kuwepo pale inafanana sana na Olvia Hitler ambaye siku zote ninaamini ni shetani ambaye alikuwa akinifwatilia
“Baba huyu ni mke wako?”
“Ndio na nimezaa naye mtoto yule mmoja”
Nikataka kuuliza jina lake ni nani ila kwenye msalaba ulio tengenezwa ukanipa jina kamili ambalo ni Olvia Abdukarim,kajasho kembamba nikahisi kina nimwagika kwenye uso wangu huku kwa mabali mapigo ya moyo yakienda kasi kiasi
“Huyu dada mimi mbona kama ninamjua”
Rahma alizungumza na kutufanya sote tumtizame na mimi wasiwasi ukazidi kunijaa na kujikuta nikikishindwa hata kuzungumza

“Umemonea wapi?”
“Sikumbuki ni wapi nimemuona ila hata majuzi nilikuwa naye ila sikumbuki ni wapi?”
“Utakuwa umeota huyu mke wangu nilimuua miaka miine ya nyuma”
“Labda watu wanafanana na pia alinielezea mambo mengi sana ila ahaaa siyakumbuki”
 Nikamtazama Rahma jinsi anavyo ishika shika picha  iliyopo kwenye kaburi hata hamu ya kuitazama ikaniishia
“Jamani mimi nipo ndani”
Nikaondoka taratibu huku nikiwaacha wakiendelea kuzungumza kuhusiana na maisha ya mke wa Mzee Ngoda,Amani yote ikatoweka moyoni mwangu ila nikaanza kujifariji kimya kimya kutokana nina pete mkononi ambayo alinipa Yudia.Wakaingia na kunikuta nikiwa nimejilaza kwenye kochi na Rahma akajiusha na kunikalia kwenye mapaja yangu
“Tutaumizana bwana”