Katika hali ya kushangaza, mwanamke mmoja raia wa Marekani ajulikanaye kwa jina la Michelle Myers ameeleza mkasa uliomkuta, kuwa alilala baada ya kusikia maumivu ya kichwa lakini alivyoamka alijikuta na lafudhi ya Uingereza.
Myers alipozungumza na Shirika la Utangazaji la CNN alieleza kuwa amewahi kufanya vipimo hospitali na kukutwa na ugonjwa wa ‘lafudhi ya kigeni’ yaani Foreign accent syndrome (FAS) ugonjwa ambao hutokana na kiharusi au majeraha katika sehemu ya lugha kwenye ubongo wa binadamu.
Kwa mujibu wa Kituo cha Magonjwa ya Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Texas huko Dallas, tatizo hili husababisha lugha mama kukabiliwa na lugha au lafudhi ya kigeni na hivyo hutokea akaweza kuongea lugha au lafudhi ya kigeni hata kama haijui na ndicho kilichomtokea Myers