Uzushi: Kujisafisha ukeni mara baada ya kufanya mapenzi huzuia mimba kutokea.  Ukweli: Mbegu za kiume zinaweza kuingia kwenye shingo ya mji wa uzazi mwanaume anapofikia mshindo, hauwezi kuondoa mbegu hizo kwa kujisafisha ukeni.
Uzushi: Mwanamke anayenyonyesha hana haja ya kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango. 

Ukweli: Mara nyingi kunyonyesha mara kwa mara na mfululizo kwa miezi 6 ya kwanza huzuia mimba. Hata hivyo sio kwa asilimia 100, kuna uwezekano mwanamke akapata mimba.
Uzushi: Mwanamke hawezi kupata mimba mara ya kwanza kufanya ngono. Ukweli: Mwanamke anaweza kupata mimba hata kama ni mara ya kwanza kufanya ngono.
Uzushi: Hauwezi kupata mimba ukifanya ngono huku umesimama. 
Ukweli: Unaweza kupata mimba hata kama ukifanya ngonoukiwa umesimama. Mbegu huingia na kufika kwenye mji wa mimba bila kujali mtindo wa mapenzi.
Uzushi: Kunywa vidonge vichache vya kuzuia mimba kabla au baada ya kufanya ngono ni njia ya uhakika ya kuzuiz mimba.
  Ukweli:Vidonge vya kuzuia mimba vinatakiwa kutumiwa kila siku ili vifanye kazi kwa ufanisi. Kunywa kabla au baada ya kufanya mapenzi kunaweza kusizuie mimba.
Uzushi: Kumwaga mbegu za kiume nje ya uke huzuia mimba kwa uhakika
Ukweli: Kiasi kidogo cha mbegu za kiume hutoka kabla ya mwanaume kufika mshindo. Mbegu hizi huweza kufika kwenye mji wa uzazi na kutunga mimba.