TCU :ORODHA YA WANAFUNZI WASIO NA SIFA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU

TCU: ORODHA YA WANAFUNZI WASIO NA SIFA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU 2016/2017
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA




TAARIFA KWA UMMA



WANAFUNZI WASIO NA SIFA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa zoezi la uhakiki wa sifa za wanafunzi wanaondelea na masomo kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu nchini kwa mwaka 2016/2017 limekamilika katika baadhi ya vyuo. Katika kutekeleza zoezi hilo Tume imebaini kuwa kuna wanafunzi ambao wamedahiliwa katika programu ambazo hawana sifa.

Orodha ya wanafunzi wasio na sifa imeshawasilishwa kwenye vyuo husika. Hivyo, wanafunzi wote wanaondelea na masomo kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu nchini wanaweza kutazama matokeo ya uhakiki wao kupitia kiunganisho (link) (Bonyeza Uhakiki wa Sifa za Udahili).

Tume inawaarifu wanafunzi wote ambao majina yao yameorodheshwa wawasiliane na vyuo vyao ili kuthibitisha sifa zao kabla ya tarehe 28 Februari 2017. Wanafunzi ambao hawatafanya hivyo hawatatambuliwa na Tume na hivyo kukosa sifa za uanafunzi.

TCU inatoa rai kwa wanafunzi wote kutembelea tovuti ya Tume (www.tcu.go.tz) mara kwa mara ili kupata taarifa mpya kuhusu uhakiki wa sifa za wanafunzi.


Kutokana na tatizo la kiufundi tembelea blog rafiki ya www.yuvinusm.blog.com kupata undani wa habari hiyo


Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?