.
Image caption: Mafuriko yaliosababishwa na Kimbunga

Watu wawili wamefariki dunia na zaidi ya 80 wameokolewa wilayani Kilwa mkoani Lindi baada ya mvua kubwa kunyesha jana Mei 4, 2024 na kusababisha mafuriko.

Kulingana na Mwananchi Digital, Mafuriko hayo mbali na kusababisha vifo, pia yamesomba madaraja na kukata mawasiliano katika eneo la Somanga.

Akizungumza leo Jumapili, Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji, Mrakibu Msaidizi Joseph Mwasabije amesema, "tumewaokoa watu 80 na wawili wamefariki dunia, ambao wote ni wakazi wa Kilwa mkoani Lindi."

Mwasabije amesema waliofariki dunia ni mwanaume na mwanamke ambao bado umri wao haujajulikana.

Wakati huohuo Mwananchi Digital imesema kwamba daraja moja limesombwa na maji na kusababisha mawasiliano kukatika kati ya mikoa ya kusini na Pwani.

Hali hiyo imetokana na madhara ya kimbunga Hidaya kilichosababisha mvua kubwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara na Kisiwa cha Mafia mkoani Pwani