Editors Choice

3/recent/post-list

MISWADA 209 YAWASILISHWA TUZO ZA UANDISHI BUNIFU

WAANDISHI bunifu 209 tayari wameshawasilisha miswada yao katika mashindano ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu ambayo yatafanyika Aprili 13,2024 ambapo ni siku ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 23, 2024, Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo hizo, Prof. Penina Mlama amesema miongoni mwa waandishi hao wapo Wafanyakazi wa majumbani, Polisi pamoja na Wauguzi wamejitosa, jambo ambalo limeonesha uwepo wa mwitikio mkubwa wa tuzo hizo ambazo kwa mara ya kwanza zilitolewa mwaka jana.

Amesema kuwa mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha sh10 milioni na kitabu chake serikali itakigharamia kukichapisha na kukisambaza mashuleni. Kwa upande wa mshindi wa pili, atapata Sh7 milioni na watatu atapewa Sh5 milioni huku washindi wa nne mpaka wa kumi watapewa vyeti kwa ajili ya kutambua ushiriki wao.
Aidha Prof. Mlama amewashukuru waandishi wa habari kwa kushiriki kutangaza tuzo hizo kwa mwaka uliopita ambapo walifanikiwa kuzipa uzito mkubwa na kutambulika ndani na nje ya nchi.

"Naomba niwashukuru sana waandishi wa habari, tuzo hii iliweza kufahamika Tanzania na nje ya Tanzania kutokana na kazi nzuri waliyoifanya waandishi wa habari, tunawashukuru sana". Amesema

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa wameongeza vipengele vya shindani ambapo kuna riwaya,ushahiri,na hadithi za watoto, tofauti na mwaka uliopita ushindani ulikuwa kwa nyanja mbili tu ambazo ni Riwaya na Ushahiri.

"Tunawajibu wa kukuza Uandishi Bunifu ambao unakuza maadili yetu na uzalendo kwa nchi yetu, lengo la tuzo hizi ni kuwatambua waandishi mahiri na malengo mengine ni kukuza lugha ya Kiswahili, kukuza utamaduni wa kujisomea , kuhifadhi historia na mitizamo bora ya Taifa la Tanzania". Amesema.

Pamoja na hayo amesema mgeni rasmi anayerajiwa kuja kutoa tuzo hizo ni Mshindi wa tuzo za Nobel kwenye uandishi wa Fasihi, Profesa Abdulazak Gurnah ambaye anaasili ya Zanzibar.

"Ushiriki wa Gurnah katika tuzo hizo kwetu kama nchi ni heshima kubwa kutokana na kujulikana duniani ,kwani kama mnakumbuka mwaka jana katika Tuzo hizi mgeni alikuwa Rais Mstaafu wa Msumbiji, Joachim Chissano ambaye ni Rais wa kwanza kuhutubia kwa lugha ya kiswahili katika mkutano wa Umoja wa nchi za Africa(AU)". Amesema Waziri Mkenda.

Naye Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET), Dkt. Anneth Komba, amesema shindano hilo ni endelevu na akiwataka watu kuendelea kuandika vitabu.

"Ni kwa kutambua umuhimu wa fasihi hata katika mitaala iliyoboreshwa serikali imeingiza somo la fasihi kwa watoto wetu hivyo vitabu vitahitajija, waandishi kazi ni kwenu kuandika vitabu vingi muwezavyo.

Aidha katika tuzo hizo amesema zaidi ya waandishi 400 kutoka ndani na nje ya nchi watahudhuria tukio hilo la utoaji tuzo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 23, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu ambayo inatarajiwa kufanyika Aprili 13,2024 ambayo ni siku ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, Prof. Penina Mlama akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 23, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu ambayo inatarajiwa kufanyika Aprili 13,2024 ambayo ni siku ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET), Dkt. Anneth Komba akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 23, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu ambayo inatarajiwa kufanyika Aprili 13,2024 ambayo ni siku ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments