Editors Choice

3/recent/post-list

MWALIMU MKUU JELA MIAKA 20 KWA KUOMBA ASALI YA MWANAFUNZI

 Novemba 30, 2022, katika Mahakama ya Wilaya Mbarali, hukumu ya Shauri la Uhujumu Uchumi Na. 16/2021 (R V ADELHARD FREDDIE MJINDO) imetolewa.

Mshtakiwa alikuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyeregete iliyopo Halmashauri ya Wilaya Mbarali, ambaye alishitakiwa kwa kosa la Rushwa ya Ngono chini ya kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ikisomwa pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi kufuatia kitendo chake cha kuomba rushwa ya ngono toka kwa Mwanafunzi wake wa darasa la 7.

Mshtakiwa aliomba rushwa ya ngono, ili amsaidie mwanafunzi huyo kufaulu mtihani wa darasa la saba.

Mahakama imemtia hatiani mshtakiwa na kumpa adhabu ya kwenda Jela Miaka 20.

Post a Comment

0 Comments