UHAKIKI WA SALAMU KUTOKA KUZIMU

IKISIRI Utafiti huu umechunguza Kutobadilika kwa Wahusika katika Riwaya Teule za Ben Mtobwa na Athari zake katika Dhamira. Riwaya hizo teule za Ben Mtobwa tulizozitumia ni Najiskia Kuua Tena na Nyuma ya Mapazia. Malengo mahsusi ya utafiti huu yalikuwa ni kuchunguza iwapo wahusika wanaojirudia katika riwaya teule za Ben Mtobwa wanabeba sifa zile zile katika riwaya zote teule, kueleza athari za kidhamira zinazosababishwa na wahusika kujirudia, kupitia uchambuzi wa riwaya teule na kubaini iwapo kuna umuhimu wa kujirudia kwa wahusika katika riwaya hizo. Data za utafiti zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya maktabani pamoja na mahojiano ambapo watafitiwa walirekodiwa kwa kutumia kinasa sauti, na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo kwa kutumia Nadharia za Saikolojia Changanuzi na Udhanaishi. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, tabia za wahusika wanaojirudia ambao ni Joram Kiango na Inspekta Kombora, zinaonekana kujirudia pia katika riwaya teule, ambazo ni Najisikia Kuua Tena na Nyuma ya Mapazia. Aidha, imebainika kuwa kumekuwa na dhamira zilizobebwa na wahusika