"Nilikuwa mdau wa kula vyakula vinavyouza barabarani hasa pweza lakini sasa sitaki kusikia kabisa,” John Marwa anasimulia mwanzo na mwisho wa kuacha kula vyakula vinavyouzwa katika maeneo ya wazi hasa barabarani na vituo vya daladala.

Vyakula maarufu vinavyouzwa katika maeneo hayo ni pamoja na chipsi, mishikaki, ndizi za kuchoma, kachori, kababu na samaki aina ya pweza ambazo baadhi ya watu wamekuwa wakidai zinaongezea nguvu za kiume.

Marwa (jina siyo halisi), mkazi wa jijini Dar es Salaam anasema ilikuwa mwaka 2021 akiwa katika moja ya kituo cha daladala akisubiri gari, ndipo alipoamua kwenda katika moja ya meza iliyokuwa na kachori, samaki aina ya pweza waliopikwa vizuri na supu yake. 

“Kama kawaida yangu nikala vipande kadhaa vya pweza na supu yake na nikapanda gari lakini hali yangu alianza kubadilika na kuanza kupata maumivu ya tumbo,” anasema Marwa.

Licha ya kuwa alifika nyumbani akijikongoja, lakini alihara sana siku hiyo na ndiyo ukawa mwisho wa kula vyakula vinavyouza katika maeneo ya wazi.

“Nilienda hospitali kesho yake, nikaambiwa huenda nilikula chakula kichafu,” Marwa anaeleza mkasa huo.

Kijana huyo ni miongoni mwa baadhi ya watu ambao ni wapenzi wa vyakula vinavyouzwa katika maeneo ya wazi. Kutokana na baadhi ya wauzaji kutozingatia kanuni za usafi jambo linalohatarisha afya za wateja wao.

Matumizi yasiyo sahihi ya maji yanayotumika kuoshea vyombo, wadudu kama nzi kugusa vyakula hivyo imekuwa sababu kubwa ya watu kupata magonjwa ya mlipuko hasa kuhara na kipindupindu. 

Shirika la Chakula  na Kilimo Duniani (FAO), limesema usalama wa chakula ni haki ya  binadamu inayotakiwa kupatikana kwa kila mtu kwa sababu kila mwaka watu 420,000 hufariki, na wengine milioni sita huugua  kutokana na ulaji wa chakula kisicho salama.

Charles Kiwia,  mkazi wa jijini hapa naye ni miongoni mwa watu ambao wanasumbuliwa maumivu ya tumbo kila akila pweza, na  kachori za barabarani .

Licha ya kujua kisababishi cha yeye kuumwa bado Kiwia anasema hawezi kuacha vyakula hivyo kwani ni vitamu mno.

“Mimi siwezi kuacha kula pweza, ni mtamu mno…nimejitahidi kuacha kula nimeshindwa kwa hiyo sasa hivi napunguza tu kipimo,” anasema Kiwia huku akibainisha kuwa anahakikisha ananunua bidhaa hiyo kwa wauzaji wanaouzingatia kanuni za usafi.

Baadhi ya samaki aina ya pweza wanaouzwa katika maeneo mbalimbali ya wazi. Picha| Gazeti App.

Kijana huyo ni miongoni mwa baadhi ya watu ambao ni wapenzi wa vyakula vinavyouzwa katika maeneo ya wazi. Kutokana na baadhi ya wauzaji kutozingatia kanuni za usafi jambo linalohatarisha afya za wateja wao.Matumizi yasiyo sahihi ya maji yanayotumika kuoshea vyombo, wadudu kama nzi kugusa vyakula hivyo imekuwa sababu kubwa ya watu kupata magonjwa ya mlipuko hasa kuhara na kipindupindu.

Shirika la Chakula  na Kilimo Duniani (FAO), limesema usalama wa chakula ni haki ya  binadamu inayotakiwa kupatikana kwa kila mtu kwa sababu kila mwaka watu 420,000 hufariki, na wengine milioni sita huugua  kutokana na ulaji wa chakula kisicho salama.

Charles Kiwia,  mkazi wa jijini hapa naye ni miongoni mwa watu ambao wanasumbuliwa maumivu ya tumbo kila akila pweza, na  kachori za barabarani .

Licha ya kujua kisababishi cha yeye kuumwa bado Kiwia anasema hawezi kuacha vyakula hivyo kwani ni vitamu mno.

“Mimi siwezi kuacha kula pweza, ni mtamu mno…nimejitahidi kuacha kula nimeshindwa kwa hiyo sasa hivi napunguza tu kipimo,” anasema Kiwia huku akibainisha kuwa anahakikisha ananunua bidhaa hiyo kwa wauzaji wanaouzingatia kanuni za usafi.

Hali ikoje kwa wauza vyakula mtaani?

Baadhi ya wauazaji wa vyakula hivyo jijini Dar es Salaam waliongea na mtandao  wanasema  wanajitahidi kufanya biashara zao katika mazingira ya usafi licha ya kuwa wanauza vyakula hivyo maeneo ya wazi ambayo yanaweza kuvutia vimelea vya magonjwa.

Mudy  Hussein, mfanyabiashara wa samaki aina ya pweza na kachori, Makumbusho Jijini Dar es Saalam, anasema anajitahidi kuhakikisha usafi  unazingatiwa wakati akiuza bidhaa ambapo huzipanga juu ya meza zikiwa wazi. 

“Kama unavyoona tunazingatia usafi, changamoto kubwa hapa ni nzi ambao nao tunajitahidi kuwadhibiti,” anasema Hussein ambaye hutumia makaratasi kuwafukuza wadudu hao akisaidiwa na mwezake.

Hata hivyo, siyo rahisi kuwadhibiti nzi wasitue kwenye chakula hicho kwa sababu hufuata shombo ya samaki.

Mfanyabiashara mwingine wa kachori na pweza jijini hapa, Karim Charles anasema amefanya biashara hiyo kwa miaka sita  sasa na tangu ameanza hajawahi kupata malalamiko kutoka kwa wateja wake kuhusu vyakula anavyowauzia.

“Hapa tunachokifanya ukipita kila meza utaona watu wawili wawili, mwingine anahudumia mwingine anafukuza wadudu na kuhakikisha usafi wa vyombo…sijawahi kupata malalamiko baada ya watu kula chakula changu ila huwa kunakuwa na changamoto za aleji,” anasema Charles. 

Licha ya wafanyabiashara hao kujitetea kuhusu huduma wanazotoa, baadhi yao hawazingatii kabisa kanuni za usafi wakati wa kuandaa vyakula hivyo.

Katika baadhi ya maeneo Nukta Habari iliyotembelea ikiwemo Mwananyamala, Mwenge na Kunduchi imekuta biashara hizo zikiwa zimezungukwa na nzi wengi. 

Baadhi ya wafanyabiashara hutumia ndoo moja yenye maji machache kuosha vyombo. Maji hayo huwa machafu na hayabadilishwi, jambo linalowaweka hatarini watumiaji wa vyakula hivyo.

Wateja wengine hutumia vijiti (toothpicks) kuchagua kachori ama pweza kisha kuchovya kwenye bakuli moja la kachumbari au pilipili. Hii inaweza kusababisha vimelea vya magonjwa kusambaa endapo kuna mtu miongoni mwao ni mgonjwa.

Madhara ya kiafya ya kula chakula kisicho salama

Ili chakula kiwe na sifa ya kutumiwa na binadamu ni lazima kiwe kimetengenzwa na kutunza katika mazingira ya safi. Ikiwa kinasafirishwa, basi kihifadhiwe katika chombo kisafi kisichoruhusu vimelea vya magonjwa.

“Kwenye maandalizi labda matunda hujaosha vizuri,au chakula hakijaiva vizuri au makontena hayajaoshwa vizuri wanaweza wakaingia wadudu kama bakteria, minyoo na protozoa,” anasema Dk Frank Leonard, kutoka hospitali ya Misigaro ya mkoani Mwanza. 

Dk Frank anasema athari za kula chakula kisicho salama zinaweza kuwa za muda mrefu au muda mfupi. Athari za kiafya za muda mfupi huanza kutokea hapo hapo na za muda mrefu huanza kujitokeza baada ya masaa 48

“Madhara ya muda mfupi ni kama kuhara na kutapika.  Madhara ya muda mrefu ni pamoja na kupata minyoo, amoeba, typhoid (homa ya tumbo),” anasema Dk Leonard.

Magonjwa haya huweza kusababisha kifo, ikiwa mgonjwa atapata madhara ya muda mrefu au muda mfupi na kushindwa kupata matibabu kwa haraka.

Ikiwa wauzaji wa vyakula vya barabarani wasipozingatia kanuni wanaweza kuchangia wateja wao kupata magonjwa ikiwemo homa ya tumbo. Picha| Muungwana Blog.

Umuhimu wa kula chakula salama ni upi?

Kwa mujibu wa ripoti ya FAO iliyochapishwa kwenye  chapisho la Mei 2022, lililopewa jina la “Fikiri kuhusu kesho ya usalama wa chakula”, faida za kula chakula salama ni pamoja na kuepuka vijidudu visababishavyo  magonjwa.

Chakula salama huokoa maisha na kupunguza magonjwa, chakula kisicho salama husababisha magonjwa mengi ikiwemo udumavu na upungufu wa viini lishe.

Uzalishaji wa chakula salama huwawezesha wazalishaji na wasambazaji kupanua wigo wa biashara kwasababu wanakuwa wamefikia matakwa ya walaji

Pia chakula salama huongeza mahudhurio kazini na kipato kwa watu wazima huku ikipunguza gharama za kutunza wagonjwa, husaidia pia kula virutubisho na  afya bora kwa muda mrefu.

Hali ikoje kwa wauza vyakula mtaani?

Baadhi ya wauazaji wa vyakula hivyo jijini Dar es Salaam waliongea na mtandao huu wanasema  wanajitahidi kufanya biashara zao katika mazingira ya usafi licha ya kuwa wanauza vyakula hivyo maeneo ya wazi ambayo yanaweza kuvutia vimelea vya magonjwa.

Mudy  Hussein, mfanyabiashara wa samaki aina ya pweza na kachori, Makumbusho Jijini Dar es Saalam, anasema anajitahidi kuhakikisha usafi  unazingatiwa wakati akiuza bidhaa ambapo huzipanga juu ya meza zikiwa wazi. 

“Kama unavyoona tunazingatia usafi, changamoto kubwa hapa ni nzi ambao nao tunajitahidi kuwadhibiti,” anasema Hussein ambaye hutumia makaratasi kuwafukuza wadudu hao akisaidiwa na mwezake.

Hata hivyo, siyo rahisi kuwadhibiti nzi wasitue kwenye chakula hicho kwa sababu hufuata shombo ya samaki.

Mfanyabiashara mwingine wa kachori na pweza jijini hapa, Karim Charles anasema amefanya biashara hiyo kwa miaka sita  sasa na tangu ameanza hajawahi kupata malalamiko kutoka kwa wateja wake kuhusu vyakula anavyowauzia. 

“Hapa tunachokifanya ukipita kila meza utaona watu wawili wawili, mwingine anahudumia mwingine anafukuza wadudu na kuhakikisha usafi wa vyombo…sijawahi kupata malalamiko baada ya watu kula chakula changu ila huwa kunakuwa na changamoto za aleji,” anasema Charles. 

Licha ya wafanyabiashara hao kujitetea kuhusu huduma wanazotoa, baadhi yao hawazingatii kabisa kanuni za usafi wakati wa kuandaa vyakula hivyo. 

Katika baadhi ya maeneo Nukta Habari iliyotembelea ikiwemo Mwananyamala, Mwenge na Kunduchi imekuta biashara hizo zikiwa zimezungukwa na nzi wengi. 

Baadhi ya wafanyabiashara hutumia ndoo moja yenye maji machache kuosha vyombo. Maji hayo huwa machafu na hayabadilishwi, jambo linalowaweka hatarini watumiaji wa vyakula hivyo. 

Wateja wengine hutumia vijiti (toothpicks) kuchagua kachori ama pweza kisha kuchovya kwenye bakuli moja la kachumbari au pilipili. Hii inaweza kusababisha vimelea vya magonjwa kusambaa endapo kuna mtu miongoni mwao ni mgonjwa.

Hatua za kuhakikisha chakula kinakuwa salama

Ripoti hiyo ya FAO imeainisha hatua tano  za kufanya chakula kiwe salama kwa matumizi nyumbani.

Hatua ya kwanza ni kuhakikisha usafi wa mikono kwani ni rahisi kwa bakteria  na vijidudu vingine kuhama kutoka kwenye mikono hadi kwenye chakula unachopika, kama hujaiosha vizuri.

Hatua ya nyingine ni kutengenisha vyakula vibichi na vilivyoiva. Vyakula vibichi mara nyingi hubeba bakteria ambao wanaweza kuingia kwenye vyakula vilivyopikwa. 

Sambamba na hayo hakikisha chakula kinaiva vizuri, kinahifadhiwa katika kiwango cha joto kinachotakiwa. Bakteria wanaosababisha sumu kwenye chakula huongezeka maradufu na haraka katika kiwango cha joto cha chini ya nyuzi joto tano na zaidi ya nyuzi joto 60. 

Weka chakula kwenye ubaridi haraka na kwa ufasaha. Ikiwezekana andika tarehe ya siku uliyohifadhi chakula kiwe kibichi au kilichopikwa.  Osha matunda na mboga kwa kutumia maji safi kabla ya kula. 

Tumia vyombo visafi kupikia na safisha maeneo ya kuandalia chakula. 

Serikali yachakua hatua kudhibiti vyakula

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mhandisi Johaness Maganga anasema shirika hilo linahakikisha wakati wote vyakula vinavyotumiwa nchini vinakuwa salama ili kuwalinda watumiaji wa mwisho ambao ni wananchi.

“TBS imeweka mifumo ya kudhibiti ili kuhakikisha chakula kilichopo sokoni nchini ni salama ili kulinda jamii kutokana na madhara ya kula chakula kisicho salama,” anasema Mahandisi Maganga.

TBS inashirikiana na wadau, wizara na taasisi mbalimbali ikiwemo Wizara ya  Uwekezaji, Viwanda na Biashara na Wizara ya Afya kuhakikisha vyakula vinavyouzwa ni salama.

Mhandisi Maganga, anasema pia wanatoa elimu kwa wananchi juu ya usalama wa chakula, kupitia vyombo vya habari, ili kuhakikisha wananchi wanatambua umuhimu wa kula chakula salama. 

Credit Nukta