TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

 OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA HANANG’

 KATESH – HANANG’. 03/04/20 -16/04/20

Descriptions

Unapojibu tafadhali taja:-

Kumb.NA.HAN/DC/E.2/1/VOLL.II/6     


Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Hanang’ imepata kibali cha ajira mbadala chenye Kumb. Na. FA.170/448/01/125 cha tarehe 05 Machi, 2020 kwa ajili ya kuajiri watumishi saba (7)kujaza nafasi ya Mtendaji wa Kijiji III.

Hivyo, Mkurugenzi Mtendaji anatangaza nafasi hizo kwa watanzania wote wenye sifa zilizoorodheshwa katika Tangazo hili wawasilishe maombi yao.


1.        AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III –NAFASI 7

SIFA ZA MWOMBAJI

Mwombaji awe na Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika Moja ya Fani zifuatazo:-

-                Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

MAJUKUMU

1.         Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
2.         Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi waUtawala Bora katika Kijiji.
3.         Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
4.         Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
5.         Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu.
6.         Kuandaa taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
7.         Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitalaam katika Kijiji.
8.         Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji.
9.         Mwenyekiti wa Kikao cha wataalam waliopo katika Kijiji.
10.     Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na Migogoro ya Wananchi.
11.     Kusimamia Utungaji wa Sheria Ndogo za Kijiji na
12.   Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

MSHAHARA:

Kwa kuzingatia ngazi za Mishahara za Serikali yaani TGS. B

MAELEKEZO YA JUMLA KWA WAOMBAJI

         i.            Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 na usiozidi miaka 45.
       ii.            Maombi yaambatishwe na taarifa ya maelezo binafsi (Curriculum vitae) ya muombaji ikioneshawadhamini watatu na taarifa zao sahihi,namba za simu za muombaji na wadhamini, cheti cha taaluma, cheti cha kidato cha nne, cheti cha kuzaliwa, na picha mbili (2) passport size (ziandikwe majina kwa nyuma ).
     iii.            Testimonial na provisional statement of results, hati ya matokeo ya kidato cha nne na sita HAVITAPOKELEWA.
     iv.            Waombaji waliostaafu / kustaafishwa au kuacha kazi katika Utumishi wa Umma hawataruhusiwa kuomba isipokuwa kwa kibali cha Katibu Mkuu kiongozi.
       v.            Muombaji atakayewasilisha taarifa na sifa za kughushi atachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa utaratibu.
     vi.            Barua zote ziandikwe kwa mkono kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza .
   vii.            Waombaji waliopo katika Utumishi wa Umma wapitishe barua zao kwa waajiri .
 viii.            Muombaji awe hajawahi kupatikana na kosa la jinai au kufungwa jela.
     ix.            Waombaji waliosoma nje ya nchi waambatishe cheti cha ulinganifu (equivalent certificate) kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania.
       x.            Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe16/04/2020.
     xi.            Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo:-


MKURUGENZI MTENDAJI WILAYA,
HALMASHAURI YA WILAYA YA HANANG,
S.L.P 2,
KATESH – HANANG’.                       


BRYCESON P. KIBASSA
MKURUGENZI MTENDAJI WILAYA
HANANG