Hivi majuzi  tarehe 8 Mei 2019, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC, ulipata taarifa za kuwepo kwa rufaa ya Serikali dhidi ya maamuzi ya Mahakama kuhusu kesi ya aliyekua Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Ndugu Abdul Nondo. 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania imekata rufaa dhidi ya kesi ya Abdul Nondo katika Mahakama Kuu ya Tanzania mkoani Iringa. Rufaa hiyo ilikatwa mahakama kuu tarehe 6/3/2019 na sababu za kukata rufaa ni hizi zifuatazo:

1) Hakimu hakuzingatia masharti ya kifungu cha 214 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai

2) Mahakama haikuzingatia ukweli kwamba upande wa mashtaka ulisibitisha mashtaka aliyoshtakiwa pasipo kuwa na mashtaka yoyote

3) Mahakama haikuzingatia Sheria kwa kuamua tofauti na maelezo binafsi ya mshitakiwa ambayo yaliwasilishwa umahakamani

4) Mahakama haikuzingatia Sheria na ukweli kuamua kwamba mshitakiwa alichukuliwa kama mshitakiwa tangu mwanzo na sio kama mlalamikaji wakati wa uchunguzi

Ingawa upande wa utetezi hawakupewa taarifa ya rufaa. Wakili wa mshitakiwa alifatilia mahakamani na kupata hati ya rufaa na kugundua kwamba serikali ilishawahi kusikilizwa mahakamani pasipo kuwepo wakili wa upande wa utetezi.

Kitendo cha mwendesha mashtaka kuendelea na rufaa pasipo kuwepo kwa upande wa utetezi ni kinyume na haki ya asili ya kusikilizwa. Ikumbukwe kwamba tarehe 5/11/2018 Mahakama ya hakimu mkazi Iringa ilimuachia huru Abdul Nondo baada ya upande wa mwendesha mashtaka kushindwa kuthibitisha pasipo kuwa na mashtaka yoyote.

Baada ya kupitia sababu za rufaa za upande wa utetezi Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umewapa maelezo wanasheria wake (Upande wa Utetezi) kuendelea na kesi ambayo tarehe ya kutajwa imepangwa kuwa 10th June 2019.katika mtandao wa Twitter Nondo ametwit kuwashukuru THRDC Kwa kukubali kusimamia rufaa hiyo.
Nondo ametweety yafuatayo







  • Nashukuru Mtandao wa watetezi Tanzania
    chini ya mratibu
    . Kwa kuwa tayari mara nyingine kusimamia rufaa iliyokatwa na Jamhuri dhidi ya kesi yangu ,pia shukrani kwa mawakili wangu
    na
    kwa kuwa tayari. Mungu awabariki