Sababu ya herufi za jina Ambulansi kuandika kutoka kulia kwenda kushoto

Kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza ni kwa nini jina katika magari ya kubebea wagonjwa wanaohitaji matibabu ya dharura almaarufu Ambulansi huwa limeandikwa kunyumenyume lakini sasa nina jibu.

Labda sio mimi pekee niliyekuwa sifahamu, najua tuko wengi tuliokuwa hatufahamu ama tulikuwa tukifahamu bila ya kuwa na uhakika.

Historia kidogo ya gari hili ni kwamba, lilianza kutumika miaka ya 1487 huko Hispania na ujio wake katika ulimwengu wa kisasa ulianza miaka ya 1830s na hadi leo gari hili ni muhimu sana katika maisha yetu.

Gari hili huwa na king’ora, wakati mwingine msalaba mwekundu na taa inayomwekamweka wakati likisafirisha mgonjwa mahututi. Na katika kila pembe huwa lina maandishi ‘Ambulance’ yaliyoandikwa kwa herufu kubwa kutoka kulia kwenda kushoto.
Siku moja niliwahi kumuuliza mtu lakini hakunijibu ni kama naye pia hakufahamu ni kwa nini huandikwa hivyo.

Madhumuni ya kuandikwa hivyo jina hilo ni kwa ajili ya kuwawilia rahisi madereva wengine mbele ya ambulansi, kusoma vyema jina hilo kupitia kioo cha dereva.

Kawaida maandishi kwenye kioo huonekana tofauti na maandishi ya kawaida na ni kwa sababu hii ni bora kuandikwa kinyumenyume ili kusomeka vyema na rahisi katika kioo.
Kila siku hasa mijini ni nadra sana kuikosa sauti ya king’ora cha gari hili la kubebea wagonjwa wa hali za dharura.
Sauti hii huwa ni ya kuwatahadharisha madereva na watumiaji wengine wa barabara kupeana nafasi kwa gari hilo kupita na kuepusha mgonjwa ambaye angeweza kuokolewa maisha kuaga dunia.

Kwa hivyo kama hukuwa na ufahamu kuhusu hilo,mtandao Wa masshele blog  umekuondolea taabu ya kujiuliza swali hilo