Wanafunzi wapatao watano wa Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda wamejikuta mikononi mwa polisi baada ya kuandamana wakipinga sheria mpya ya mitandao ya kijamii inayowataka raia wote wa Uganda wanaotumia mitandao hiyo kutozwa kodi.

Mtandao wa gazeti la New Vision la nchini Uganda limeandika kuwa wanafunzi hao waliandamana juzi July 2, 208 ambapo walikuwa wanaandamana kuelekea bungeni.

Uganda imepitisha rasmi sheria ya kutoza kodi kwa watumiaji wote wa mitandao ya kijamii, na sheria hiyo imeanza kufanya kazi July 1, 2018.