Baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza kuanza mchakato wa kumsaka kocha mpya wa Taifa Stars, Mbelgiji, Adel Amrouche ameibuka na kufunguka kuwa, ak­ipewa nafasi ya kuinoa timu hiyo, ataipam­bania ishiriki Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar. 

 Mbali na Kombe la Dunia, pia Mbelgiji huyo mwenye asili ya Algeria, amesema ataanza kwanza kupambana kuhakiki­sha Taifa Stars inashiriki Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) inayotarajiwa ku­fanyika mwakani nchini Cameroon.

 Hivi karibuni, Kaimu Ka­tibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred, alisema mchakato huo wa kumsaka kocha, unaendelea vizuri ambapo wanaanza kupitia wasifu ‘CV’ mbalimbali za mako­cha walioomba nafasi hiyo baada ya kocha wa sasa, Salum Mayanga kumaliza mkataba wake tangu mwezi uliopita.

 Amrouche aliyezaliwa Machi 7, 1968 katika Mji wa Kouba, Algiers nchini Algeria, amesema: “Nina uzoefu na soka la Afrika, nimefundisha timu ya taifa ya Kenya na Burundi, lakini pia kwenye klabu, nimefundisha DC Motema Pembe ya DR Congo na USM Alger ya Algeria.

 “Najiamini na ndiyo maana nimekuwa nikitam­ani sana kuifundisha Taifa Stars ambayo imekuwa na kiu kubwa ya mafanikio, kama nikifanikiwa kuwa kocha wa timu hiyo, nita­hakikisha mwakani tuna­shiriki Afcon, kisha 2022 lazima twende kushiriki Kombe la Dunia.

Hayo yote yanawezekana kwani ikiwekwa mikakati mad­hubuti nadhani hakuna kitakachoshindikana.”

CHANZO: CHAMPIONI