2.3. Namna za Utamkaji

Utamkaji wa sauti za lugha unategemea sanajinsi hewa inavyopita kutoka mapafuni hadi kufikia kwenyemkondo-sauti. Iko migawanyo mikuu kadhaa inayotofautisha sauti kwa njia hii.
i) Ughuna
Katika kongomeo kuna nyuzi-sauti ambazo zinakuwa katika nafasi za aina mbili wakati hewa inapopita. Ikiwa nyuzi-sauti ziko pamoja (yaani zimekaribiana au kusogeana karibu) hewa inapotoka kwenye mapafu huzisukuma na kuzitenganisha wakati wa kupita, na hivyo kusababishamsukumo. Sauti zinazotolewa wakati huu zinakuwa na mghuno na huitwa sauti ghuna. Ikiwa nyuzi-sauti hizi zimeachana, hewa hupita kwa urahisi bila kuzuiliwa, na hivyo bila kusababisha msukumo. Sauti zinazotolewa wakati huu huwa hazina mghuno, na huitwa sighuna. Sauti zifuatazo ni baadhi ya zile zinazoitwaghuna: [b, d, g, d, z, m, n, v]. Sautisighuna ni kama [p, t, k, q, Å¡, è, f].
Kwa kawaida irabu huwa ni ghuna, ingawa zipo lugha chache ambazo zinatofautisha kati ya irabu ghuna na irabu sighuna. Hivyo irabu sighuna huonyeshwa kwa kuwekewa alama bandikizi [o] au [] chini ya alama za irabu kama: [a, i, u], kuzitofauitsha na irabu ghuna [a, i, u]. Konsonati, kama tulivyoonyesha hapo juu, zinaweza kuwa ghuna au sighuna.
ii) Ung’ong’o
Wakati wa utoaji sauti, kaakaa laini linaweza kuwa katika nafasi za aina mbili. Ikiwa limeteremshwa au kushushwa nyuma ya koo, njia inayokwenda kwenye tundu la pua huachwa wazi, na hivyo hewa inaweza kupita puani wakati buo huo ikipitia kinywaai. Sauti zitakazotolewa wakati huu zitakuwa na ung’ong’o, na zinaitwa sauti ng ‘ong ‘o. Sauti hizo ni kama [m, n, h]. Sauti sing’ong’o kama vile [b, p, g, k, d, t] n.k. hutolewa wakati kaakaa laini limeinuliwa na hivyo kufunga njia inayokwenda kwenye tundu ia pua na kufanya hewa ipite kinywani tu. Mara nyingi sauti ng’ong’o pia ni ghuna, lakini zipo lugha zilizo na sauti ngo’ng’o ghuna na sighuna katika mifumo yake ya fonolojia. Sauti ng’ong’o sighuna hutofautishwa na ghuna kwa kuwekewa alama bandikizi [o] kama za irabu sighuna hapo juu. Kwa kawaida katika lugha nyingi, irabu huwa sing’ong’o. Hata hivyo katika lugha chache zipo tofauti za msingi kati ya irabu ng’ong’o na sing’ong’o. Ung’ong’o katika irabu huonyeshwa kwa kuwekewa alama bandikizi [~] au [^] juu: [â, î, u] na hivyo kuzitofautisha na irabu ghuna ambazo ni sing’ong’o: [a, i, u].
iii) Mpwnuo
Sauti pumuo hutokea wakati utamkaji huandamana na fumba la pumzi kutoka kinywani. Kwa kawaida mpumuo hutokea pamoja na sauti sighuna, na hutokea katika mifumo sauti ya lugha nyingi. Huonyeshwa kwa kuwekewa alama [h] juu ya sauti inayoandamana nayo kama [ph, kh, th] na hivyo kutofautishwa na zile ambazosipumuo kama [p, k, t].
iv) Mzuio
Wakati hewa inapopita kinywani, inaweza kuzuiliwa au kutozuiliwa, na hivyo kusababisha tofauti katika sauti zinazotolewa. Kwa kawaida katika utamkaji wa irabu, hewa inapita bila kuzuiliwa, ambapo utamkaji wa konsonanti huandamana na mzuio wa hewa.
Konsonanti zinaweza kugawanywa katika vikundi kufuatana na aina ya mzuio, na kutuwezesha kutofautisha kati ya sauti ambazo mpaka wakati huu tumeziweka katika kundi moja.
a) Vipasuo Hewa inapopita kinywani, kunaweza kutokeamzuio-kamili wa mkondo-hewa kwa muda mfupi, halafu hewa ikaachiliwa ghafla. Sauti zinazotolewa wakati huu huitwavipasuo, nazo ni kama [b, p, d, t, g, k].
b) Vikwamizi Katika utoaji wa sauti za namna hii, mkondo sauti unazuiliwa nusu tu, na hivyo hewa inapita kwa kujisukuma kupitia katika nafasi au uwazi mdogo uliopo, na hivyo kusababisha kukwamakwama. Sauti za namna hii huitwa vikwamizi, na baadhi yake ni [f, v, qd, s, z, Å¡, ]. Ni rahisi kuona tofauti kati ya vipasuo na vikwamizi kwa kuweka mkono mbele ya kinywa wakati wa kutamka vipasuo, na halafu wakati wa kutamka vikwamizi. Utagundua kuwa wakati wa kutamka sauti kwamizi kama [s, f] unahisi hewa ikisukumizwa.
c) Vipasuo-kwamizi Hizi ni sauti ambazo hutolewa kwa kuchanganya mzuio wa muda mfupi (kama katika vipasuo) na mzuio nusu unaosababisha ukwamizi. Sauti hizi ni kama [è, j].
d) Vilainisho au vimadende Sauti [l, r] zinaitwa vilainisho. Ingawa wakati zinapotolewa kunakuwa na mzuio wa mkondo-hewa kama katika utoaji wa konsonanti nyingine, mzuio huu ni mdogo sana na hausababishi ukwamizo. Wakati sauti [l] inapotolewa, ulimi huwa umeinuliwa na kugusana na ufizi, na hivyo hewa hupita kwa kuzunguka kwenye pembe za ulimi. Sauti [r] hutolewa kwa kukunja ncha ya ulimi nyuma ya ufizi.
e) Viyeyusho Hizi ni sauti ambazo ziko katikati ya irabu na konsonanti, na mara nyingi huitwairabu-nusu. Wakati zinapotolewa, kuna mzuio mdogo sana wa mkondo-hewa. Zikitokea katika neno, kwa kawaida zinatanguliwa na kufuatwa na irabu. Wakati wa kuzitamka, ulimi husogea haraka haraka kutoka au kuelekea kwenye irabu iliyo karibu. Sauti hizi ni [j, w] kama katika maneno <yai, watu>. Tofauti kati ya sauti hizi na irabu ni kuwa hazipewi usilabi, ambapo irabu zote zinapewa usilabi.
Kielelezo II: Baadhi ya Konsonanti

Midomo
Mdomo-
meno
Meno
Ufizi
Kaa kaa
gumu
Kaa kaa
laini
Glota








Pasuo







-sighuna
p


t

k

-sg pumuo
ph


th

kh

-ghuna
b


d

g









Ng’ong’o
m


n
ñ
h









Kwamizi







-sighuna

f
q
s
Å¡


-ghuna

v
d
z

g









Pasuo-







Kwamizi







-sighuna




c


-ghuna




j










Yeyusho







-sighuna






h ?
-ghuna




j
w









Laini-







sho




1 r